Home Burudani Lulu: Sifurahii ugumba

Lulu: Sifurahii ugumba

871
0
SHARE
Elizabeth Michael ‘Lulu’

NA KYALAA SEHEYE,

STAA wa filamu za Bongo anayeshikilia taji la msanii bora wa kike Afrika alilotwaa nchini Nigeria Machi mwaka huu nchini Nigeria, Elizabeth Michael ‘Lulu’, amesema anakerwa anaposikia mtu anaitwa mgumba, kwani linaumiza sana na kudhalilisha.

Lulu ameyasema hayo kufuatia kutumika sana kwa neno hilo miongoni mwa jamii, hasa wasichana wanaodhani ugumba unaletwa na mtu mwenyewe, ilhali kupata mtoto ni mipango ya Mungu.

Msanii huyo tangu apate tuzo hiyo amekuwa akitoa ushauri mbalimbali kwa jamii, ambapo pia amekuwa akikemea tabia ya wasichana kujiingiza katika ulevi na kuyafanya maisha yakose mwelekeo.

“Nashangaa sana neno ugumba limekuwa likitumika kudhalilishana wakati hili lina mpango wa Mungu ndani yake, kwa kweli sipendelei jina hilo,” alisema.

Kwa upande wake Lulu, alisema kwamba yeye bado umri wake unamruhusu kuendelea kufanya mambo yake na muda wa kuwa na familia utakapowadia atafanya hivyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here