Home Habari LWANDAMINA ATUMA SALAMU COMORO

LWANDAMINA ATUMA SALAMU COMORO

747
0
SHARE

NA MARTIN MAZUGWA


KLABU ya Yanga imepiga hesabu za mbali kwa kutumia Kombe la Mapinduzi kama maandalizi ya Ligi ya Mabingwa Afrika yanayotarajia kuanza Februari mwaka huu ambapo itaanzia ugenini katika visiwa vya Comoro.

Vijana hao wa Jangwani wameanza kwa kishindo michuano hiyo baada ya kuishushia kichapo cha mabao 6-0 timu ya Jamhuri ya Pemba, ikiwa ni salamu tosha kwa wapinzani wao wanaowafuatilia kwa kina klabu ya  Ngaya Club de Mde ya Comoro.

Kocha wa timu hiyo, George Lwandamina, tayari ameanza kulifanyia kazi zaidi eneo la ushambuliaji ambalo linaongozwa na Donald Ngoma,  Emanuel Martin, Amissi Tambwe pamoja na Simon Msuva, ambao wamekuwa moto wa kuotea mbali katika mashindano ya Mapinduzi.

Tayari Ngoma na Msuva wamefungua akaunti ya mabao kwa kishindo mara baada ya kila mmoja kupachika mabao mawili na kuongoza  katika orodha ya wafungaji katika mashindano hayo.

Kocha Lwandamina ambaye hivi sasa amekuwa akiangalia wachezaji ambao watamfaa kwenye kikosi cha kwanza na kutengeneza mfumo atakaoutumia katika mashindano ya kimataifa, amekuwa akiwapa nafasi wachezaji wake wote ili kuangalia viwango vyao.

Yanga itaanza kutupa karata yake ya kwanza michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya timu ngeni katika mashindano hayo ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu ya Comoro, Ngaya club de Mde, huku Yanga ikiwa na historia ya kufanya vizuri pindi inapokutana na timu zinazotoka katika visiwa hivyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here