Home Burudani MADEE: NAPENDA KUENDESHA GARI JIPYA KILA SIKU

MADEE: NAPENDA KUENDESHA GARI JIPYA KILA SIKU

392
0
SHARE

NA BEATRICE KAIZA

MSANII anayefanya vizuri katika tasnia ya muziki wa Bongo Fleva nchini, Hamadi Ally ‘Madee’ , amejipatia umaarufu kupitia nyimbo zake mbalimbali,, ukiwemo unaotamba kwa sasa ‘Vuvula’ aliomshirikisha Temba ambao umekuwa kielelezo cha sanaa katika Taifa letu.

Madee, ambaye anapendwa na mashabiki wengi kutokana na mashairi mazuri ya nyimbo zake, ameongea na safu hii na kueleza baadhi ya mambo ambayo yamekuwa ni sehemu ya maisha yake.

NAPENDA KUENDESHA GARI MPYA KILA SIKU

“Kwenye maisha yangu kitu ambacho ninakipenda ni kuendesha gari jipya kila siku, hicho ndicho ninachokipenda, pia napenda kuwa na furaha kila wakati, kuwa na amani muda wote.

ASICHOKIPENDA

“Katika maisha yangu sipendi dharau, sipendi kumdharau mtu yeyote, awe mkubwa awe mdogo kwangu wote sawa, sipendi majungu na ndiyo maana mimi mwenyewe huwezi kunikuta namsema mtu, pia nachukia kuendesha gari bovu.

CHAKULA

“Nikiwa nyumbani chakula ninachopendelea kula ni ugali mlenda na samaki wa kukaangwa, hakuna chakula ninachokipenda kama hiki.

ANACHOPENDA AKIWA NYUMBANI

“Nikiwa nyumbani napenda sana kuangalia TV, hasa kipindi cha mpira, napenda sana kuangalia mpira uwe wa Tanzania au wa nje, ilimradi uwe mpira wa miguu napenda kuangalia.

MTU WAKE WA KARIBU

“Yaani nikiwa na matatizo yangu binafsi watu wangu wa karibu ni wazazi wangu, nawapenda sana wazazi wangu, ndiyo maana wanakuwa mstari wa mbele katika matatizo yangu, pia mwanangu Saida naye nikiwa na tatizo nikiongea naye tu naridhika.

MATUMIZI YAKE KWA SIKU

“Yaani huwezi amini mimi kwa siku huwa natumia pesa ndogo sana, huwa natumia elfu kumi tu kuanzia asubuhi hadi jioni na inatosha kabisa bila wasiwasi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here