Home Michezo Kimataifa MADRID KUIKATIA RUFAA KADI NYEKUNDU YA RAMOS

MADRID KUIKATIA RUFAA KADI NYEKUNDU YA RAMOS

682
0
SHARE

MADRID, Hispania

KLABU ya Real Madrid inajipanga kuikatia rufaa kadi ya pili ya njano aliyooneshwa nahodha na beki wao, Sergio Ramos, katika mchezo dhidi ya Deportivo uliochezwa wikiendi iliyopita.

Mwamuzi wa mchezo huo, Jose Luis Gonzalez, alijikuta akitupiwa lawama na mashabiki wa Madrid, baada ya kumuonesha kadi ya pili ya njano Ramos na kuzaa nyekundu, lakini mabingwa watetezi hao wa La Liga wanajipanga kuikatia rufaa.

Ramos alioneshwa kadi hiyo kufuatia kitendo cha kumpiga kiwiko mchezaji wa Deportivo, Fabian Schar, wakati timu yake ikiibuka na ushindi wa mabao 3-0.

Aidha, ripoti ya mwamuzi huyo ilisema: “Ramos aliinua mkono wake na kumpiga mpinzani wake kwa kiwiko kwa namna isiyopendeza.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here