Home Habari Mahadhi wa Coastal awaita Simba mezani

Mahadhi wa Coastal awaita Simba mezani

373
0
SHARE

Coastal UnionNA SAADA SALIM

KIUNGO wa Coastal Union, Juma Mahadhi amesikia fununu kuwa Simba wanamuhitaji naye ametamka wazi kuwa mpira ni kazi yake na kamanda hachagui pori hivyo kama Wekundu hao wa Msimbazi hawatanii juu ya jambo hilo waweke mezani Mill. 60 hatakuwa na kipingamizi.

Tayari inasemekana Yanga wameshaanza mazungumzo na kiungo huyo kwa ajili ya kukiimarisha kikosi chao msimu ujao lakini na mchezaji mwenyewe amewaambia Simba bado wanayo nafasi ya kumchukua kama watachangamkia dili.

Alisema mazungumzo yake na Yanga hayafungi kuzungumza na klabu nyingine kwani hajaingia mkataba nao hivyo kama Simba wanataka huduma yake wala haina neno kabisa, waweke tu Mil 60 mezani.

“Hizo taarifa za Simba kunihitaji ndiyo kwanza nazisikia, ninachoweza kukuambia ni kwamba Yanga ndio pekee waliokuja rasmi kwangu na tupo kwenye mazungumzo.

“Hata hivyo kama Simba wananihitaji bado wanayo nafasi kwani sijaingia mkataba wowote na Yanga, mimi naweza kucheza popote ilimradi taratibu zifuatwe,” alisema.

Akizungumzia ushindani wa namba katika timu hizo kubwa alisema mpaka wanaanza kumtafuta wameona uwezo wake hivyo anaweza kupambana popote bila tatizo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here