Home Uncategorized Maisha ya Tanzania yamnogea Nimubona

Maisha ya Tanzania yamnogea Nimubona

573
0
SHARE

EMERYNIMUBONA-1NA SAADA SALIM

MKATAA kwao ni mtumwa, usemi huu na mingine hutumika sana na huwa una maana yake hasa pale unapotuliza kichwa na kuanza kuzidadavua.

Je, mnajua nani huyo? Ni beki wa kulia wa Simba Mrundi, Emery Nimubona, baada ya uongozi wa klabu hiyo kuonyesha nia ya kumtema tayari beki huyo ameanza mchakato wa kusaka timu hapa hapa nchini.

Simba ambao wameonyesha dhahiri kutomuhitaji mchezaji huyo licha ya kuendelea kufanya siri juu ya wachezaji ambao wataachwa na kusajili kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Nimubona ambaye yuko nchini kwao Burundi tayari ameshahamisha familia yake hadi Tanznaia ambapo amesema kwamba akili na mwili viko Tanzania hata kama akiwa hayupo hapa nchini.

Breaking News lilifanikiwa kufanya mazungumzo na beki huyo maarufu kwa jina la Kadogo, ambapo alieleza mambo mbalimbali ikiwemo na mustakabali wake msimu ujao.

Mustakabali baada ya kutemwa

Nimubona anasema baada ya kupokea taarifa za kutemwa kwake katika kikosi cha Wekundu wa Msimbazi, Simba, hafikirii kucheza soka nchini kwao Burundi.

“Katika akili yangu kwa sasa sijawaza suala la kucheza soka hapa nyumbani, bado natamani kucheza soka Tanzania hivyo kuna uwezekano wa kurejea tena ila si Simba.

“Simba wameniacha lakini kuna timu nafanya nayo mazungumzo, kwa sasa kutaja ni timu gani itakuwa mapema baada ya kila kitu kikiwa sawa nitazungumza,” anasema.

Beki huyo anasema iwapo ikitokea bahati mbaya amekosa timu Tanzania bado ataendelea kuikumbuka ila dhamira yake ni kucheza soka Tanzania ila ikishindikana basi atalazimika kurudi Burundi katika klabu ya Athletico Olympic aliyokuwa akiitumikia zamani.

Alichojifunza Simba

Beki huyo anasema kuna vitu alivyojifunza kutoka timu hiyo, lakini jambo ambalo hataweza kulisahau kuona timu hiyo ikiendeshwa bila ya kuwa na mipango endelevu.

“Kikosi cha Simba kilikuwa na wachezaji wazuri, lakini viongozi hawakuwa na msimamo pamoja na uvumilivu katika benchi la ufundi hivyo kila mtu anahitaji kuongoza timu hali ambayo imetufanya kushindwa kufanya vyema katika mechi zetu za mwisho,” anasema.

Madai yake Simba

Nimubona anasema licha ya kutomwambia jambo lolote lakini bado anaidai Simba fedha zake za usajili kutokana na kutomaliziwa fedha hizo kipindi ambacho anasaini mkataba wa miaka miwili kutumikia timu hiyo.

“Ninaidai Simba, lakini wameshindwa kuniambia jambo lolote, kutokana na sipendi fujo nimeamua niachane nalo na kuhangaika na masuala la maisha yangu,” anasema Nimubona ambaye kwa sasa yupo mapumziko kwao Burundi.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here