SHARE

NA EZEKIEL TENDWA

HUENDA Simba wakapata pigo kubwa baada ya kiungo wao Mzimbabwe, Justice Majabvi, kuweka wazi kwamba ataifuata familia yake nchini Austria na sasa anatafuta timu ya kuchezea nchini humo.

Awali uongozi wa Simba ulikuwa unahangaika kumshawishi kiungo huyo kuendelea kukipiga kwao lakini juhudi hizo zimegonga mwamba.

Taarifa za kuaminika zinadai kuwa Majabvi kwa sasa anafanya kila linalowezekana kutafuta timu nchini humo ili kuungana na mkewe ambaye anafanya kazi nchini humo.

Majabvi amekuwa mmoja wa wachezaji tegemeo ndani ya kikosi cha Simba kutokana na uwezo wake wa kucheza namba zaidi ya moja ambapo kuondoka kwake kutakuwa pengo kubwa.

Kiungo huyo anamudu pia kucheza kama beki wa kati ambapo mara kadhaa linapotokea pengo alikuwa akirudishwa kusimama kati na aliyekuwa kocha wa muda wa kikosi hicho Mganda, Jackson Mayanja, aliwahi kumsifu mchezaji huyo kwamba ana nidhamu ya hali ya juu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here