SHARE

 

Jastice MajabviNA SAADA SALIM

BEKI wa kimataifa wa Simba, Mzimbabwe Jastice Majabvi, ametimkia nchini Sweden kusaka nafasi ya kucheza soka la kulipwa huku pia akimvuta kiungo wa timu hiyo, Abdi Banda.

Majabvi ameondoka juzi nchini na ilikuwa aondoke na Banda lakini inaelezwa kiungo huyo wa Simba amesitisha safari hiyo mpaka baada ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kumalizika.

Licha ya kwenda kuweka sawa mipango ya kucheza soka nchini humo, Majabvi ametumia fursa hiyo kwenda kupumzika na familia yake ambayo inaishi Sweden.

Banda alipoulizwa na DIMBA kuhusu mpango huo alikiri kuwa upo na kwamba  muda wowote atatimka zake mambo yatakapokamilika.

“Hii safari nilitaka kwenda na Majabvi ambaye ameenda Sweden kwa mke wake, na pia nikuambie tu kwamba kuna timu nyingine kubwa tu ya nchini Qatar nayo imeonyesha nia ya kunichukua hivyo nasubiri taarifa kutoka kwa wakala wangu ambaye anafuatilia kila kitu.”

“Bado sijajua ni timu gani naenda kuchezea lakini muda si mrefu kila kitu kitakuwa sawa kwani wameniambia nisubiri hadi Agosti. Kuhusu suala la kuongeza mkataba Simba sijakuwa na maamuzi sahihi mpaka sasa na kama ikitokea nitasaini miezi sita tu,” alisema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here