Home Habari MAJEMBE MTIBWA FITI KUIVAA SIMBA

MAJEMBE MTIBWA FITI KUIVAA SIMBA

916
0
SHARE

NA JESSCA NANGAWE

KUREJEA kwa wachezaji watatu wa Mtibwa Sugar waliokuwa majeruhi kumeleta matumaini makubwa ndani ya kikosi hicho na sasa kipo katika maandalizi ya mwisho kabla ya mchezo wao dhidi ya Simba mwishoni mwa juma hili.

Mtibwa inatarajia kutua jijini Dar es salaam keshokutwa tayari kwa pambano lao dhidi ya Simba, mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru.

Akizungumza na DIMBA kocha wa timu hiyo, Zubeiry Katwilla, alisema anashukuru kuona wachezaji wake Shabaan Kado, Hassan Isiaka pamoja na Haruna Chanongo wakiwa wamerejea kwenye afya zao baada ya kukosa takribani mechi tano za ligi kuu msimu huu.

“Tunajiandaa vizuri, kikosi changu kipo tayari kuwavaa Simba, natambua utakuwa mchezo mgumu unaohitaji umakini mkubwa, ukiangalia Simba tumefungana pointi kwenye msimamo wa ligi, hivyo kila timu itakuwa ikisaka ushindi kwa nguvu,” alisema Katwilla.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here