Home Habari MAKAMBO AACHA SIMULIZI SHINYANGA

MAKAMBO AACHA SIMULIZI SHINYANGA

2074
0
SHARE

NA MASYENENE DAMIAN

STAILI ya straika wa Yanga, Heritier Makambo ya kushangilia pale anapofunga bao, imekuwa gumzo mkoani Shinyanga kutokana na watu wa rika mbalimbali kuiiga.

Licha ya kwamba kikosi chake hicho kilifungwa bao 1-0 na Stand United, lakini hiyo haikuwazuia vijana kwa watoto kuonyesha staili hiyo ya ushangiliaji ya kujaza upepo.

Makambo ambaye aliingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Haruna Moshi ‘Boban’, ndiye anayeongoza kwenye mbio za ufungaji akiwa na mabao 11 huku akitamba na staili yake hiyo ya ushangiliaji.

Hicho ni kipigo cha kwanza kwa Yanga kupoteza tangu ligi ianze lakini bado wanashika usukani wakiwa na pointi 53 ambapo kocha wao, Mwinyi Zahera, ametamba kuwa mapambano yanaendelea.

Wapinzani wao wa jadi Simba, wako nafasi ya nne wakiwa na pointi 33, nafasi ya pili wakiwa Azam FC, huku nafasi ya tatu wakikaa KMC ambao huu ni msimu wao wa kwanza kupanda daraja.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here