SHARE

NA TIMA SIKILO

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Heritier Makambo, ametamba kutinga fainali za Kombe la Shirikisho la Azam (FA).

Katika kuitafuta nafasi hiyo, Yanga wanatarajiwa kukutana na Lipuli kesho, kwenye mchezo wa nusu fainali utakaopigwa Uwanja wa Samora, mkoani Iringa.

Endapo Yanga itashinda itatinga hatua ya fainali na kucheza na Azam FC, ambayo imeshaingia fainali baada ya kuiondoa KMC ya Kinondoni kwa ushindi wa bao 1-0.

Akizungumza na DIMBA jana, Makambo alisema siku zote mchezo wa soka hauhitaji maneno, lakini wanaimani watakapokutana dakika 90 zitaongea.

Alisema anaamini wana nafasi kubwa ya kutinga fainali hizo kutokana na mazoezi ya nguvu wanayoendelea nayo na pia ari ya kushinda mechi hiyo waliyokuywa nayo wachezaji wote.

ìTunaweza kufanya vizuri dhidi ya Lipuli na huenda tukakutana na Azam kwenye fainali kwa sababu kila mmoja anahitaji hiyo nafasi,î alisema.

Azam juzi walifanikiwa kutinga nafasi hiyo baada ya kuitoa KMC kwa bao 1-0, hivyo Lipuli au Yanga yeyote anaweza kwenda kuungana na Azam kucheza fainali hizo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here