SHARE

MWAMVITA MTANDA

MASHABIKI waliota- rajia kumuona Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, katika jukwaa la wageni rasmi jana walipigwa na butwaa baada ya kiongozi huyo kukaa katika benchi la wachezaji wa akiba wa Simba.

Makonda ambaye anajiweka wazi kuwa ni mwanachama wa Simba, alijichanganya na wachezaji wa akiba huku akipiga stori na kiungo wa timu hiyo Jonas Mkude.

Tukio hilo licha ya kuonyesha kuwashangaza mashabiki, lilinogesha kilele cha tamasha la SportPesa Simba Week jana Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam likiwa sasa linatimiza miaka 10 tangu lilipoanzishwa.

Sherehe hizo zilihitimishwa na mechi ya kimataifa ya kirafiki ambapo Simba iliifunga Power Dynamos ya Zambia mabao 3-1 huku shujaa akiwa Meddie Kagere.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here