Home Burudani MALAIKA KUJA NA STYLE MPYA

MALAIKA KUJA NA STYLE MPYA

4400
0
SHARE

NA JESSCA NANGAWE


MREMBO aliyefanya vyema na ngoma ya ‘Zogo’ Malaika amefunguka na kusema ukimya wake utarudi na kishindo cha aina yake kwani anajipanga kuachia kitu kipya wakati wowote ambayo itamtofautisha na alipotoka.

Malaika ambaye amekua kimya kwa muda sasa tangu wimbo wake wa Zogo ufanye vyema kwenye soko la burudani amesema wakati wowote wimbo wake wa ‘Haachi’ utakua hewani ukiwa na taswira tofauti kama alivyozoeleka.

“Unajua unapokaa kimya kwa muda halafu ukataka kurudi kila shabiki atatamani kuona unarudi vipi, sitaki wanione Malaika yule yule kuna mambo mengi mapya ya ubunifu nimeongeza kwenye kazi zangu na hata mwonekano wangu utakua tofauti”alisema Malaika

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here