SHARE

MANCHESTER, England

KLABU ya Manchester City huenda ikakumbana na adhabu ya kufungiwa usajili kufuatia uhamisho wao wa kinda la Argentina, Benjamin Garre kutoka Velez Sarsfield.

Velez waliwasilisha malalamiko yao FIFA Septemba mwaka jana wakidai City ilivunja kanuni za usajili walipomshawishi mchezaji huyo akiwa chini ya umri uliowekwa kwenye kanuni na sasa City wanatarajiwa kupandishwa Mahakama ya Michezo (CAS).

Klabu hiyo ilidai kuwa City ilizungumza na Garre alipokuwa na umri wa miaka 15 kabla ya kumsajili alipofikisha miaka 16.

Hata hivyo, FIFA ilitupilia mbali malalamiko hayo kwani wanaziruhusu klabu zilizo ndani ya Umoja wa Ulaya kusajili wachezaji wadogo na Garre alikuwa na ‘passport’ ya Italia.

Lakini maofisa wa Velez walisema kuwa City ilivunja kanuni kwa sababu Garre aliicheza klabu hiyo akiwa Argentina na jana walitarajiwa kuwasili CAS sasa watapelekea malalamiko hayo CAS ifikapo Julai 3, mwaka huu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here