Home Habari Manara aingia chaka Taifa

Manara aingia chaka Taifa

1719
0
SHARE

NA ABDULAH MKEYENGE

UMEWAHI kuona mtu akipotea kwao? Ndivyo ilivyomtokea Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba Hajji Manara alipoingia Uwanja Taifa na moja kwa moja kwenda katika jukwaa la mashabiki wa Simba na kukutana na mashabiki wa Yanga, huku wale wa Simba wakikaa upane wa Yanga.

Ni kwenye mchezo wa hisani ulioandaliwa wa mastaa Mbwana Samatta (Mchezaji) na Ali Kuba (Msanii) ukiwa na mlengo wa kuchangisha fedha kwa ajili ya watoto wenye uhitaji maalum, ulimkuta Manara akikutana na wakati huo mgumu.

Manara alikuwa Ofisa Habari wa Team Samatta na team Sammata ikakaa upande wa Yanga na Team Kiba wakikaa katika jukwaa la Simba, hivyo Manara alivyoingia alikwenda moja kwa moja jukwaa la Team Kiba alipokutana na wakati mgumu wa kuzomewa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here