Home Habari MANULA AIOTA TUZO YA KIPA BORA

MANULA AIOTA TUZO YA KIPA BORA

607
0
SHARE

NA JESSCA NANGAWE,

KIPA namba moja wa Azam FC, Aishi Manula, amesema ana nafasi kubwa ya kutwaa tuzo ya kipa bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, kutokana na kusimama vema langoni mwa timu yake.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Manula alisema kwamba, dhamira yake ni kutwaa tuzo hiyo kwa sababu ni moja ya malengo yake msimu huu, ndiyo maana amekuwa akifanya vizuri.

“Mpaka sasa tumeruhusu goli moja tu kwenye mzunguko huu wa pili, hii kwangu inanipa faraja kubwa ya kusema ninaweza kuibuka kipa bora, nadhani safu yangu ya ulinzi unasimama vizuri, ndiyo maana hata mimi naonekana bora,” alisema.

Katika mzunguko huu wa lala salama, Manula ameruhusu bao moja tu, mingine yote akisimama vizuri langoni, kitu ambacho kinampa jeuri ya kusema ataibuka kipa bora.

Katika hatua nyingine, Manula alisema licha ya wadau wengi wa soka kuzipa nafasi timu za Simba na Yanga kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, lakini wao bado hawajakata tamaa, ndiyo maana wanatafuta pointi tatu katika kila mchezo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here