Home Habari MANULA: AZAM MNISAMEHE

MANULA: AZAM MNISAMEHE

545
0
SHARE

NA CLARA ALPHONCE,

BAADA ya kudaiwa kusaini mkataba wa miaka miwili ndani ya Simba, kipa wa Azam FC, Aishi Manula, amesema ameondoka katika timu hiyo akiwa bado anaipenda, pia amewaomba radhi kwa maamuzi yake magumu aliyochukua.

Akizungumza na DIMBA, Manula alisema kwamba, Azam ni timu ambayo imemlea toka akiwa mdogo mpaka hadi hivi sasa, hivyo anaiona kwamba ni shehemu ya familia yake, ila kinachomwondoa ni suala la kutafuta maslahi zaidi.

“Ni kweli Azam wamenitoa mbali, hilo lazima nikiri, lakini wakati umefika wa kuondoka kutokana na maslahi. Ingawa niseme wazi kwamba hii ni timu niliyoipenda na nitaendelea kuipenda daima.

“Watu wanaongea mengi kuhusu mimi kujiunga na timu nyingine kuwa hawalipi mishahara kwa wakati. Mimi naelewa kuwa timu hizi kubwa zina matatizo yake, kwa hiyo nimejiandaa kisaikolojia na kukubaliana na kila hali nitakayokutana nayo,” alisema Manula, ambaye kwa sasa yupo kwenye majukumu ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, inayoshiriki michuano ya Kombe la Cosafa, nchini Afrika Kusini.

Manula ni mmoja wa wachezaji waliokuzwa na Azam na baadaye kuwa tegemeo kwenye kikosi cha kwanza, kisha Taifa Stars, ambaye ameamua kuachana na timu hiyo, huku akieleza kuwa kinachomwondoa ni maslahi pamoja na kushiriki michuano ya kimataifa, ambayo Simba inashiriki msimu ujao kwenye Kombe la Shirikisho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here