SHARE

NA JESSCA NANGAWE

BAADA ya kudaiwa kutoka kimapenzi na staa mwenzake wa muziki wa Bongofleva Mimi Mars,msanii Marioo amekiri kuwa habari hizo zimemchafua kwa kiasi kikubwa.

Marioo ambaye amekua akifanya vyema katika kazi zake amesema si kweli kama aliwahi kutoka na mrembo huyo lakini kukuzwa kwa taarifa hizo kwa kiasi kikubwa zimemuweka kwenye wakati mgumu ndani ya familia yake na mahusiano yake ya sasa.

“Sidhani kama skendo ya mimi kutoka kimapenzi na Mimi Mars imenisaidia kitu, labda tu naweza kusema imenipunguzia baadhi ya vitu mitaani, lakini nafkiri kila kitu kinakuja kwa sababu zake, ukweli imeniweka kwenye njiapanda sana hasa kwa familia yanguîalisema Marioo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here