Home Michezo Kimataifa MARTIAL AKIFUNGA NA MONACO WANAFUNGA

MARTIAL AKIFUNGA NA MONACO WANAFUNGA

349
0
SHARE
Anthony Martial

MANCHESTER, England

KAMA ni furaha basi tufurahi wote. Huo ni msemo rahisi unaoweza kuutumia katika suala hili linalomhusu winga Anthony Martial na klabu ya AS Monaco.

Martial kwa sasa anakipiga katika klabu ya Man United, alitua hapo akitokea Monaco miezi 18 iliyopita kwa dau la euro miloni 40, lakini makubaliano ya nyongeza za malipo kwa Monaco bado yanaendelea kutimizwa baina ya klabu hizo.

Tangu alipotua United, Martial amepachika jumla ya mabao 24 na iwapo atafunga bao lingine kesho dhidi ya St. Ettiene kwenye Ligi ya Yuropa, kiasi cha euro milioni 10 kitaingia kwenye akaunti ya Monaco kutimiza makubaliano.

Euro milioni 10 nyingine zitaenda huko kama Martial atafikisha mechi 25 kwenye timu yake ya Taifa ya Ufaransa, ambako hadi sasa amecheza mechi 15 na euro milioni 10 zitamiminika kwa Monaco kama winga huyo atafanikiwa kuingia kwenye tatu bora ya orodha ya watakaowania tuzo ya Ballon d’Or.

Wakati Martial akifurahia bao lake, Monaco nao watakuwa wamefunga bao lao, wataingiza pesa tu kwenye akaunti.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here