SHARE

LOS ANGELES, Marekani

HIYO ilitokea juzi, mara tu msanii huyo wa muziki wa hip hop alipoposti picha iliyouonesha mkono wake ukiwa umeshika mguu wa mtoto ambaye hata hivyo uso wake haukuonekana.

Ghafla, sehemu kubwa ya mashabiki wa kike wa rapa huyo mwenye umri wa miaka 34, walionesha kukerwa, kila mmoja akisema alitamani kuwa mama wa watoto wa Trey Songz.

Shabiki anayefahamika kwa jina la Suz kupitia ukurasa wake wa mtandao wa twitter aliandika: “Wow, nimeumia kuona Trey Songz na mtoto mzuri kama huyo na mtu mwingine ambaye si mimi.”

Mwingine anayekwenda kwa jina la delamey aliandika: “Ooooo, nitakuwa na huzuni kubwa sana kwa sababu ana mtoto na mtu ambaye si mimi…”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here