Home Habari MASHABIKI WAZIMIA UWANJANI

MASHABIKI WAZIMIA UWANJANI

1072
0
SHARE

NA SAADA SALIM,

MASHABIKI wa Simba na Yanga jana walizimia uwanjani wakati timu hizo zilipocheza mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliomalizika kwa Wekundu hao wa Msimbazi kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Kwa mujibu wa Katibu wa Chama cha Madaktari wa Michezo (TASMA), Nasor Matuzya, idadi ya mashabiki waliozimia ilikuwa 18, ambapo kati ya hao, mmoja aligundulika akiwa na ugonjwa wa degedege na mwingine ugonjwa wa moyo.

“Ni kweli tulipata wagonjwa hao na kati yao wanne walipelekwa katika Hospitali ya Temeke, ambapo mmoja aligundulika kuwa na ugonjwa wa degedege na mwingine ugonjwa wa moyo na mwingine akisumbuliwa na kichwa na mpaka sasa (jana) kuna mmoja amepoteza fahamu na bado hajazinduka,” alisema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here