SHARE

NA MWANDISHI WETU

BAADHI  ya mashabiki wa Yanga SC wameutaka uongozi wa  Klabu hiyo kumtupia virago Kocha Mkuu wa timu hiyo Mwinyi Zahera kutokana na  mwenendo mbaya wa timu hiyo katika Ligi Kuu Bara na michuano ya Kimataifa.

Wawakilishi hao  wa Tanzania katika michuano ya  Kombe la Shirikisho Afrika jana walichezea kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa FC Pyramids ya Misri.

Kipigo hicho cha jana kimetibua  nyongo za mashabiki hao na kutaka Zahera awajibike kwani kwani timu hiyo mpaka sasa haina mwelekeo wa kufanya vyema kwenye Ligi na hata mechi ya marudiano dhidi ya Waarabu hiyo.

Wakizungumza na DIMBA, mara baada ya mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, mashabiki hao walisema, Zahera ameishiwa mbinu za kuinoa timu hiyo na ni wakati muafaka uongozi ukafanya maamuzi magumu dhidi yake.

Walisema,kuendelea kumng’ang’ania kocha huyo ni kuiangamiza timu hiyo na huenda wakasusia kwenda uwanjani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here