SHARE

NA JESSCA NANGAWE

WENYE Yanga yao utawambia nini tena wakakuelewa kama si kuipa sapoti timu yao? Ndiyo ilivyo kwa mashabiki zaidi ya 300 ambao wanatarajia kuwa sehemu ya majukwa ya Uwanja wa Levy Mwanawasa mjini Ndola, Zambia.

Tayari msafara wa mashabiki hao ulianza safari jana kwenda nchini humo ukitumia mabasi ya kawaida, lengo likiwa ni kuongeza hamasa katika pambano hilo muhimu kwa timu yao pendwa.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz, alisema mashabiki hao walitarajiwa kuanza safari jana saa saba mchana kwa kutumia mabasi ya kawaida, huku wengine wakijumuika katika mikoa mbalimbali.

“Ili kuongeza hamasa, mashabiki mbalimbali wataungana na sisi viongozi kwenye mchezo huu wa marudiano na siku moja kabla ya safari tayari mashabiki waliojiorodhesha walikua ni wengi ambao idadi yao ni zaidi ya 300, tunaamini wataongeza hamasa katika pambano hili,” alisema Nugaz.

Kikosi hicho kilitarajiwa kutua jana usiku katika mji mkuu wa Zambia, Lusaka, baada ya kubadili msimamo wao ambao awali walipanga kwenda moja kwa moja mjini Ndola na sasa wamefanya hivyo ili kukwepa hujuma za wapinzani wao.

Yanga itarudiana na Zesco mwishoni mwa juma hili katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kukubali sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza uliyofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here