Home Habari MASTRAIKA SIMBA, YANGA WAFUNIKWA HAT-TRICK

MASTRAIKA SIMBA, YANGA WAFUNIKWA HAT-TRICK

261
0
SHARE

NA WINFRIDA MTOI,

ZIKIWA zimesalia mechi chache kabla ya msimu wa 2016/17 kumalizika, kuna uhaba wa mabao matatu ‘hat-trick’, wakati pia hakuna mchezaji yeyote kutoka Simba au Yanga aliyeingia kwenye rekodi hizo.

Ni hat-trick mbili pekee zilizofungwa hadi sasa msimu huu, tofauti na hat-trick saba zilizofungwa msimu uliopita.

Hat-trick ya kwanza msimu huu ilifungwa na Kelvin Sabato ‘Kevi Kiduku’ wa Majimaji, katika mzunguko wa kwanza wakati huo akiitumikia Stand United.

Katika mchezo huo dhidi ya Mtibwa Sugar ya Manungu, Morogoro iliyomalizika kwa sare ya 3-3, Kevi Kiduku alifunga mabao yote matatu.

Hii ni hat-trick iliyodumu kwa muda mrefu msimu huu hadi mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo Abdulrahamani Mussa wa Ruvu Shooting alipachika mabao matatu na kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Majimaji.

Msimu uliopita, mshambuliaji wa Yanga, Amis Tambwe, alifunga hat-trick mbili, ya kwanza ikiwa ni ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Stand United na mabao 5-1 dhidi ya Majimaji.

Naye mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajib, aliifungia mabao matatu timu yake ikishinda 6-1 dhidi ya Majimaji, huku aliyekuwa mshambuliaji wa Simba, Hamis Kiiza, pia akipachika mabao yote matatu katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Kagera Sugar.

Wengine waliofunga hat-trick msimu uliopita ni Mbaraka Yusuph wa Kagera Sugar katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Coastal Union, Waziri Junior aliyeisaidia Toto Afrika kushinda mabao 5-1 dhidi ya Majimaji na Salim Aziz ‘Gilla’ wa Mgambo Shooting iliyoshuka daraja, wakishinda mabao 5-1 dhidi ya JKT Ruvu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here