Home Habari MAVUGO, BOCCO WAANZA KAZI RASMI

MAVUGO, BOCCO WAANZA KAZI RASMI

559
0
SHARE

NA SAADA SALIM,

MASTRAIKA wa Simba, Laudit Mavugo na John Bocco wameingia vitani kila mmoja akijifua kivyake kuhakikisha anaifanyia timu yake mambo makubwa katika mechi za ligi za zile za kimataifa, pindi msimu utakapoanza.

Mavugo yupo nchini kwao Burundi ambapo anajifua vikali kuhakikisha hakuna anayemuweka benchi, huku Bocco naye akipambana jijini Dar es Salaam kwenye mazoezi ya Gym.

Bocco amesajiliwa na Simba akitokea Azam FC ambapo hataki kusikia kabisa suala la kukaa benchi na Mavugo naye anapambana kuhakikisha kocha mkuu wa kikosi hicho, Joseph Omog, anamwamini na kumpanga mara kwa mara.

Katika safu ya ushambuliaji ya Simba, kwa sasa ina changamoto kubwa kutokana na usajili uliofanywa akiwamo Emmanuel Okwi, huku pia wakihusishwa kutaka kumshusha Straika wa Nkana FC ya Zambia Walter Bwalya.

DIMBA lilimtafuta Mavugo ambapo alisema tangu alipofika nchini kwao alikuwa katika mapumziko ya mwisho wa msimu lakini, amekuwa akijifua vikali kujiweka sawa kwa ajili ya msimu ujao.

“Unapokuwa mchezaji unatakiwa mara kwa mara ufanye mazoezi na hilo ndilo ninalopambana nalo huku, najifua kujiweka sawa na kwa sasa nasubiri Simba wanitumie tiketi kwa ajili ya kurejea Tanzania,” alisema Mavugo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here