Home Habari Mayanja anukia Mwadui

Mayanja anukia Mwadui

928
0
SHARE

NA SALMA MPELI

KOCHA msaidizi wa Simba Mganda, Jackson Mayanja, ametajwa kumrithi aliyekuwa kocha wa Mwadui, Jamhuri Kihwelu ‘Julio’, aliyetangaza kujiuzulu kufundisha timu hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita.

Akizungumza na DIMBA jana, Katibu wa Mwadui, Ramadhan Kilao, alisema kwa sasa bado uongozi haujaanza mazungumzo na kocha yeyote kwa ajili ya kuchukua nafasi ya Julio, lakini jana walitarajiwa kufanya kikao cha pamoja ili kujadili suala hilo.

Alisema kwa sasa timu itakuwa chini ya kocha msaidizi, Mwanamtwa Kihwelu, hadi pale watakapoamua ni kocha gani anaweza kuchukua nafasi hiyo.

“Julio ameamua mwenyewe kuachia timu, lakini hakuwa ametoa tamko rasmi na leo jioni (jana), tutakuwa na kikao naye kwa ajili ya kujua kama anaondoka rasmi ili kuamua ni kocha gani atachukua nafasi yake.

“Suala la kuanza mazungumzo na Mayanja si kweli kwani kila mtu anazungumza lake na hatuwezi kuzungumza na kocha mwingine wakati bado hatujakaa na Julio kujua mustakabali wake ndani ya timu,” alisema Kilao.

Mayanja ambaye kwa sasa yupo kwao nchini Uganda, imetajwa kuwa hiyo ni moja ya mipango yake kwa ajili ya kujiunga na timu hiyo ya Mwadui.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here