Home Michezo Kimataifa MAYWEATHER AAMUA KUJIITA TBE

MAYWEATHER AAMUA KUJIITA TBE

273
0
SHARE

LOS ANGELES, Marekani

BINGWA asiyepigika mwenye maneno mengi,  Floyd Mayweather  Jr,  aliyecheza mapambano 49 na kushinda yote, ameamua kubadili jina na kuanza kujiita TBE (The Best Ever), yaani mkali wa milele.

Mkali huyo alisema ataanza kulitumia jina hilo kuanzia sasa, kauli ambayo aliitoa alipokuwa katika ziara ya kitalii nchini Uingereza.

“Pindi unapozungumzia mabondia wakongwe  unataja mabondia bora waliocheza  michezo zaidi ya 100, lakini ukiangalia rekodi mimi nimewapiga  mabondia bora zaidi katika historia ya ngumi,” anasema.

Mayweather, mwenye  umri wa miaka 40, alistaafu kucheza masumbwi mara baada ya kumtwanga Andre Berto katika pambano lililopigwa mwaka jana na kuhitimisha safari yake katika mchezo wa masumbwi  kwa kushinda mapambano 49, huku 26 yakiwa kwa KO.

Bingwa huyo ameamua kurudi  ulingoni kuzipiga na mkali wa ngumi mchanganyiko, Connor McGregor, ambaye mara kwa mara amekuwa akitamba kuvunja rekodi ya mkali huyo ya kutopoteza pambano.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here