Home Habari MBAO WANUSA REKODI YA YANGA

MBAO WANUSA REKODI YA YANGA

987
1
SHARE

NA MAREGES NYAMAKA,

UNAKUMBUKA ile mvua ya mabao iliyowakuta Kagera Sugar kutoka kwa mabingwa watetezi Yanga na kuwafanya kuweka rekodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu kwa kufungwa mabao 6-1? Sasa timu ya Mbao wamejibu mapigo kwa kutaka kunusa rekodi hiyo ambayo bado haijavunjwa hadi sasa.

Mbao ilijibu na kunusa rekodi ya mabao 6-1, baada ya kuifunga Mtibwa Sugar mabao 5-0 matokeo ambayo yamewashtua mashabiki wengi wa soka kutokana na ukweli kwamba Mbao ni wageni wakati Mtibwa ni timu kongwe kwenye ligi.

Kocha wa Mbao, Etienne Ndayiragije, amesisitiza kwamba matokeo hayo hayakuwa rahisi kupatikana kwa sababu kulikuwa na ushindani mkali ila anafurahi kwa sababu rekodi yao kama timu ngeni kwenye ligi wameiweka.

“Ni kitu cha kushukuru kupata ushindi mkubwa namna hiyo, tena kwa timu ambayo ina uzoefu mkubwa na sisi tukiwa tunashiriki kwa mara ya kwanza, nadhani hii itakuwa chachu ya kufanya vizuri michezo yote iliyobakia,” alisema.

Mbao FC ambao ni mara yao ya kwanza kushiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, waliibuka na ushindi huo dhidi ya wakata miwa hao mchezo uliochezwa katikati ya wiki hii Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here