SHARE

NA MAREGES NYAMAKA

SIKU chache baada timu ya Stand United kupata udhamini wa Sh milioni100, majirani zao Mbao FC pia wamepata bonge la udhamini wa Sh milioni 70 sambamba na gari la kisasa litakalowasaidia kusafirisha timu.

Akizugumza na DIMBA Jumatano, Mwenyekiti wa klabu hiyo, Solly Zephania, amewashukuru wadhamini wao hao wapya na kudai kitendo hicho kitawapa chachu ya kufanya vizuri zaidi msimu huu.

“Ni kweli tumepata udhamini mpya wa mwaka mmoja wenye thamani ya jumla ya shilingi milioni 140, kutoka Kampuni ya uagizaji magari na kusafirisha mizigo ya GF Trucks & Equpments, ambapo mgawanyo wake wanatupa pesa taslimu shilingi milioni 70 na inayosalia wanatukabidhi basi jipya la thamani hiyo,” alisema.

Aliongeza kuwa wamefarijika sana hasa upande wa gari ambalo litawasaidia sana kwa safari za kwenda kucheza mechi za ugenini mikoani, kwani hilo lilikuwa ni moja ya mambo yaliyokuwa yakiwakwamisha.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here