SHARE

Tima Sikilo

MSHAMBULIAJI wa timu ya Azam FC, Mbaraka Yusuph, amesema anahofu ya kurudi uwanjani lakini baada ya muda atazoea na atarudi kwenye kiwango chake.

 Mbaraka ameanza mazoezi na kikosi chake baada ya kukaa nje ya uwanja takribani mwaka mmoja akiuguza majeraha ya goti.

Baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti lake la mguu wa kulia Aprili mwaka jana katika Hospitali ya Vincent Pallotti jijini Cape Town, Afrika Kusini, kufuatia kubainika kuchanika mtulinga wa kati wa goti hilo.

Akizungumza na DIMBA Jumatano,Mbaraka alisema,maendeleo yake ni mazuri na anafanya mazoezi ya nguvu baada ya kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu kutokana na kuuguza goti hivyo anarudi uwanjani akiwa na hofu ya kuumia tena.

“Namshukuru Mungu nimerudi kwenye timu na ninafanya mazoezi na wenzangu , ushindani wa namba upo ila sina hofu na hilo kitu ambacho kinaniumiza kwasasa ni hofu ya kuumia ukizingatia nimekaa nje muda mrefu.”alisema Mbaraka Yusuph.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here