SHARE

NA SAADA SALIM

STRAIKA wa Kagera Sugar, Mbaraka Yussuf, amechaguliwa mchezaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Machi kwa msimu wa 2016/2017.

Katika mechi tatu ambazo Kagera Sugar iliyocheza Machi mwaka huu, Mbaraka alisaidia kupata matokeo ikiwemo mchezo wa mwisho wa ligi kuu dhidi ya Simba ambapo alifunga bao moja kati ya 2-0 iliyoyapata ilipowakaribisha Simba kwenye Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.

Katika mabao ya Kagera Sugar, straika huyo amefunga mabao 11 huku akiipeleka hadi nafasi ya tatu timu yake kwa kuishusha Azam FC ambayo kwa sasa ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi.

Mbaraka aliwashinda wachezaji, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ wa Azam FC na Kenny Ally wa Mbeya City kutokana na kuonyesha kiwango kizuri.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here