Home Habari Mbaya wa TP Mazembe atua Jangwani

Mbaya wa TP Mazembe atua Jangwani

1219
1
SHARE

Javier Besala BokunguNA SAADA SALIM

UNAMKUMBUKA Javier Besala Bokungu? Yule mchezaji aliyeiharibia TP Mazembe hadi ikatolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2011 na nafasi yake kuchukuliwa na Simba?

Ngoja nikukumbushe kidogo, ishu ilikuwa hivi; Simba ilicheza na TP Mazembe mwaka huo na kutolewa kwa jumla ya mabao 6-2, ikifungwa 3-1 ugenini na kuongezwa kipigo kingine cha mabao 3-2 hapa nyumbani. Wekundu hao chini ya aliyekuwa Mwenyekiti, Ismail Aden Rage, hawakukubali wakakata rufaa na kushinda ambapo TP Mazembe ikaondoshwa kwenye michuano hiyo kwa kwa kosa la kumchezesha mchezaji batili, Janvier Besala Bokungu, raia wa Jamhuri ya Congo (DRC).

Kwa mujibu wa CAF, Kamati ya Mashindano ilibaini kuwa TP Mazembe, ilifanya kosa kwa mujibu wa kifungu nambari VIII kinachohusiana na ulaghai wa kumchezesha Bokungu.

Amini usiamini sasa mchezaji huyo yuko nchini na wakati wowote atamwaga wino kukipiga katika klabu ya Jangwani, Yanga.

Yanga imeamua kufanya kweli kwa kusainisha majembe ya ukweli ili kukiongezea nguvu kikosi chao kitakachoshiriki michuano ya Kombe la Shirikisho ambapo baada ya kufanikiwa kumsainisha Hassan Ramadhan ‘Kessy’ sasa wamevuka mipaka na wanataka kufanya usajili wa kushtukiza kutoka nchini Congo.

Mbali na Bokungu ambaye anamudu vema kucheza namba zaidi ya moja na ambaye aliwahi kukipiga katika Klabu ya Esperance ya Tunisia, pia imemvuta mkali mwingine, Mussa Ndusha kutoka klabu ya DC Motemapembe, pia ya Congo.

Bokungu anao uwezo wa kucheza kama beki wa kati, beki wa kulia pamoja na nafasi ya kiungo huku Ndusha naye akimudu vema nafasi ya kiungo wa kati, winga zote mbili kulia na kushoto anamudu, lakini pia ni mzuri akicheza kama straika wa mwisho.

Taarifa za uhakika zilizolifikia DIMBA zinadai kwamba, wachezaji hao tayari wametua hapa nchini wakiwa wamefichwa maeneo ya Mbezi Beach chini ya wakala wao anayeitwa Kimanda ambaye ni mdogo wa beki wa zamani wa Yanga, Constantine Kimanda.

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here