SHARE

NA SAADA SALIM


STRAIKA wa Stand United, Alex Kitenge ambaye aliifunga Yanga hat-trick, ameitwa kwenye kikosi cha vijana cha U-23 cha Burundi lakini familia yake imemkatalia.
Burundi wanaratajia kuingia kambini Novemba 6 mwaka huu kujiandaa na mchezo wa kufuzu Afcon U23 dhidi ya Ngorongoro Heroes mchezo utakaochezwa Novemba 20 mwaka huu Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na DIMBA, Kitenge alisema amezuiliwa na baba yake kuitumikia timu ya taifa ya nchi hiyo kutokana na uraia wa wazazi wake kutokea DR Congo.
“Novemba 5 tunaingia kambini, lakini natakiwa niende nyumbani kwanza kumsikiliza mzee, kwani hataki kusikia nabadili uraia wa Congo.
“Naiheshimu na napenda kuchezea Burundi kutokana na kujulikana kwangu na kunifanye niwe hapa, lakini msimamo wa mzee kwangu imekuwa shida na nitaenda kusikiliza matakwa yake,” alisema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here