Home Habari MBELGIJI ATAKA REKODI KWA KMKM

MBELGIJI ATAKA REKODI KWA KMKM

921
0
SHARE

NA MWANDISHI WETU, ZANZIBAR

BAADA ya kuiangushia kichapo cha mabao 4-1 Chipukizi ya Zanzibar, Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, amesema leo KMKM nao watatafuta pa kutokea kwani amewaandalia dozi ya maana.

Wekundu hao wa Msimbazi, watacheza mchezo wao wa pili leo Uwanja wa Amaan Zanzibar, dhidi ya KMKM katika mfululizo wa michuano ya Mapinduzi iliyoanza katikati ya wiki hii.

Akizungumza na DIMBA jana, Aussems alisema amewaambia wachezaji wake wahakikishe wanaibuka na ushindi mnono ili kuzidi kujitengenezea rekodi ya kushinda mabao mengi kuliko timu nyingine yoyote.

“Najua utakuwa mchezo mgumu kwani hata wapinzani wetu wanataka kuondoka na pointi tatu, lakini wachezaji wangu wanajua umuhimu wa kuendeleza wimbi la ushindi.

“Tunataka ikiwezekana tupate ushindi mwingine wa mabao mengi na tuwe timu pekee iliyoshinda kwa idadi kubwa ya mabao, hapo ndipo kocha anapima ubora wa kikosi chake ulipo,” alisema.

Alisema anataka msimu huu Simba …

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la DIMBA.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here