SHARE

mbeya-cityNA ZAINAB IDDY

UONGOZI wa timu ya Mbeya City kutoka mkoani Mbeya, imewapiga chini wachezaji wake saba ambao walikuwepo kwenye msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliomalizika hivi karibuni akiwamo Themi Felix ‘Mnyama’.

Katibu mkuu wa kikosi hicho, Emmanuel Kimbe, amelithibitishia DIMBA Jumatano kuwa wanaachana na wachezaji hao kwani wameshindwa kuendana na kasi yao.

Alisema wachezaji ambao wamemaliza mikataba yao na wana mipango nao ya baadaye wameshaanza nao mazungumzo ili kuangalia namna ya kuwaongezea mkataba.

“Tumeachana na wachezaji saba ambao tayari mikataba yao imefika ukingoni, lakini pia kwa mujibu wa ripoti ya kocha haitaji kuendelea nao, hivyo tunawapa ruhusa ya kutafuta timu nyingine.

“Lakini pia wapo ambao mikataba yao imekwisha na hawapo kwenye orodha hiyo, hawa tutaongea nao kwa lengo la kuwapa mikataba mipya,” alisema.

Kikosi hicho kinachonolewa na kocha Mmalawi, Kinnah Phiri, msimu uliopita kilimaliza ligi kikiwa katika nafasi ya nane baada ya kujikusanyia pointi 35 kibindoni katika michezo 30 waliyocheza.

Wachezaji walioachwa na timu hiyo ni pamoja na kipa, Haningtony Kalyesubula ambaye tayari anahusishwa kuwa na mazungumzo na Simba, walinzi Yusuph Abdallah, Deo Julius, Hamad Kipo,  Yohana Morris, Richard Peter na mshambuliaji, Temi Felix ‘Manyama’.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here