SHARE

MWANDISHI WETU, Dar es Salaam
KATIKA kuadhimisha Siku ya Ukimwi Duniani Desemba Mosi mwaka huu, Umoja wa Wakazi wa Mbezi Beach umeandaa mbio za kujifurahisha, maarufu ëMbezi Fun Runí, zitakazorindima siku hiyo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mratibu wa mbio hizo, Omary Kimbau, alisema, mbio hizo za kuanzia Kilomita tano, 10 na 21, zitaanzia katika Hoteli ya Ramada Kunduchi, jijini Dar es Salaam.
Alisema mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.
Kimbau alisema lengo la kuandaa mbio hizo ni kubadilishana mawazo, kufahamiana na kusaidiana kwenye shida na raha, huku kauli mbio ikiwa ëUsibweteke, tumia condom, ngoma bado ipoí.
Kwa upande wake, Msanii wa zamani wa kundi la maigizo la Kaole, Christina Manongi, maarufu Sinta, alisema katika bonanza hilo kutakuwa na burudani mbalimbali kutoka kwa Bendi ya K- Mondo Sound na Up town Entertaiment, watakaopiga muziki kwa washiriki watakaojitokeza siku hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here