Home Habari MBONDE OUT, BOCCO IN OKTOBA 28

MBONDE OUT, BOCCO IN OKTOBA 28

1232
0
SHARE

NA SAADA SALIM

SIMBA itamkosa beki wake kisiki, Salum Mbonde, katika mchezo dhidi ya Yanga, utakaochezwa Oktoba 28, mwaka huu, kutokana na majeraha yanayomkabili, lakini straika John Bocco atakuwa fiti kuitumikia timu hiyo yenye maskani yake Mtaa wa Msimbazi, Dar es Salaam.

Taarifa kutoka ndani ya Simba ambazo Dimba inazo ni kwamba, Mbonde ana majeraha ambayo hayatamruhusu kucheza Oktoka 28, kwa sababu bado atakuwa hajawa sawa sawa, hivyo kuwa miongoni mwa wachezaji wa Simba watakaoikosa mechi hiyo kubwa Tanzania.

Aidha, Bocco atalazimika kuukosa mchezo wa mwishoni mwa wiki hii dhidi ya Njombe Mji, utakaochezwa Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam, ikiwa ni hatua za kujiweka sawa kabla ya kuivaa Yanga.

“Bocco atakosa mchezo mmoja dhidi ya Njombe Mji, lakini Mbonde atakosa michezo minne, Njombe Mji, Yanga, Mbeya City na Tanzania Prisons na baada ya hapo tunaamini atarudi mzigoni,” kilisema chanzo chetu.

Mbali na Mbonde na Bocco, wachezaji wengine majeruhi ni pamoja na kipa Said Mohamed ambaye anatoka kupatiwa matibabu nchini India, pamoja na Shomari Kapombe, ambao hawajaonja ladha ya Ligi Kuu msimu huu tangu wasajiliwe na Simba kwa sababu walikuwa kwenye matibabu.

Wawili hao waliumia katika mchezo uliopita dhidi ya Mtibwa Sugar, uliomalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1, uliochezwa Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here