SHARE


NA EZEKIEL TENDWA


WAKATI Yanga wakitoa dozi kwa timu za Morogoro walikoweka kambi, wenzao Simba wametoa ratiba ya mechi zao nne za kirafiki huko Afrika Kusini walikokwenda kunoa makali yao.

Yanga walianza kutoa dozi ya mabao 10-0 dhidi ya Tanzanite, mchezo wa kwanza kabla ya Ijumaa ya wiki hii kuifunga tena Moro Kids mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Chuo cha Biblia, mkoani Morogoro.

Yanga wao wakiwa wanaendelea kuzifunga timu za Morogoro, wenzao Simba wametoa ratiba ya michezo minne watakayocheza huku Sauz, ikiwamo na timu kubwa ya Orlando Pirates inayonolewa na kocha wa zamani wa Wanajangwani hao, Milutin Sredojevic maarufu kama ‘Micho’.
Simba wataanza kibarua chao hicho dhidi ya Orbret TVET ya nchini Afrika Kusini, mchezo utakaochezwa Jumanne ya wiki ijayo, kabla ya kucheza tena dhidi ya Platinum ya nchini humo siku inayofuata yaani Julai 24.

Julai Julai 27 Simba watacheza dhidi ya Township Rollers ya Botswana ambayo iliwahi kuitoa nishai Yanga michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2018 na Julai 30 watamaliza dhidi ya Orlando Pirates.

Wekundu wa Msimbazi hao wameweka kambi kwenye hoteli ya Royal Marang katika Mji wa Rustenburg, wakitumia Uwanja wa Bafoken Sports Campus, kufanyia mazoezi.

Baada ya michezo hiyo, watarejea nchini kujiandaa na tamasha lao ya Simba Day litakalofanyika Agosti 8 mwaka huu, huku mashabiki wao wakisubiri kwa hamu kubwa utambulisho rasmi wa wachezaji wao wa msimu unaokuja.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here