SHARE

BUENOS AIRES, Argentina

NAHODHA wa timu ya Taifa ya Argentina, Lionel Messi, ameondolewa kwenye ratiba ya kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Morocco wiki ijayo, ikiwa ni hatua ya tahadhari baada ya kupata maumivu ya nyonga.

Messi alikumbana na tatizo hilo wakati akiitumikia Argentina dhidi ya Venezuela mwishoni mwa wiki hii, mtanange uliomalizika kwa vigogo hao wa Amerika Kusini kubamizwa mabao 3-1.

Kichapo hicho walichokipata Argentina kilikuwa ni cha kwanza kwa Messi tangu alipojiondoa kwenye timu hiyo baada ya kumalizika kwa fainali za Kombe la Dunia mwaka jana.

Aidha, hatua ya Messi kutocheza mechi dhidi ya Morocco, itamsaidia nyota huyo kujiweka fiti kabla ya kuiongoza Barcelona dhidi ya Man Utd, kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, itakayochezwa Aprili 10.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here