Home Habari Messi apumzishwa kisa Man United

Messi apumzishwa kisa Man United

1376
0
SHARE

CATALUNYA, Hispania

STAA wa kikosi cha Barcelona, Lionel Messi, alipumzishwa katika mchezo wao wa Ligi Kuu ya Hispania dhidi ya Huesca hapo jana.

Lakini imebainika kuwa nyota huyo raia wa Argentina hayupo vizuri tangu alipopata jeraha la jicho katika mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Manchester United ambao Barcelona walishinda bao 1-0.

Kabla ya kurudiana na vijana wa Ole Gunnar Solskjaer, walicheza dhidi ya Huesca katika mchezo ambao mpaka gazeti hili linaingia mtamboni mechi ilikuwa bado haijaanza.

Pia, kiungo wa Barcelona, Sergio Busquet, naye alitazamiwa kupumzishwa kwenye mchezo huo ili kupata nguvu mpya ya kupambana na viungo wa Manchester United katika mchezo wa marudiano.

Barcelona wanaongoza Ligi Kuu ya Hispania kwa pointi 11 zaidi ya wanayemfuatia huku ikiwa imebaki michezo saba ligi hiyo kumalizika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here