Home Michezo Kimataifa MESSI HATARINI KUFUNGIWA

MESSI HATARINI KUFUNGIWA

308
0
SHARE

LA PAZ, Bolivia

NAHODHA wa Argentina, Lionel Messi, mwishoni mwa wiki alifunga bao kwa njia ya penalti kuweza kuipa timu yake ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Chile, katika mechi ya Kanda ya Amerika Kusini kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2018 huko Russia, lakini imedaiwa kwenye mechi hiyo staa huyo alimshambulia mshika kibendera, Marcelo Van Gasse kwa matusi makali katika kipindi cha pili.

Na baada ya mechi hiyo, inasemekana Messi alikataa kumpa mkono mwamuzi huyo msaidizi.

Hata hivyo, tukio hilo halikuwekwa kwenye ripoti ya awali ya mwamuzi wa kati wa mechi, lakini baadaye likaongezwa na kupelekwa kwenye Shirikisho la Soka kwa nchi za Marekani ya Kusini (CONMEBOL).

Na usiku wa kuamkia na jana kilichokuwa kikingojewa ni uamuzi wa Kamati ya Nidhamu ya CONMEBOL, ambayo ilikuwa ikisubiriwa kutoa adhabu mara moja, hivyo Messi kuikosa Mechi ya Argentina na Bolivia huko La Paz, ama kuamuru kifungo kiwe baada ya mechi hii.

Hata hivyo, kitendo cha Argentina kukata rufaa ndicho kingemwezesha Messi kucheza na kifungo chake kutumika baada ya rufaa kuamuliwa, ikiwa atashindwa na mechi itakayohusika ni ya mwezi Agosti dhidi ya Uruguay.

Hivi sasa Argentina wapo nafasi ya tatu kwenye kundi hili la Kombe la Dunia 2018, wakiwa nyuma ya vinara Brazil na Uruguay.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here