Home Habari MEXIME AICHIMBA MKWARA YANGA

MEXIME AICHIMBA MKWARA YANGA

808
0
SHARE

NA JESSCA NANGAWE

KOCHA wa Kagera Sugar, Mecky Mexime, amesema haihofii hata kidogo Yanga kwa kuwa anakifahamu vyema kikosi hicho kinachonolewa na Mzambia George Lwandamina, huku akiamini ushindi wao wa kwanza utapatikana kwenye mchezo huo.

Yanga na Kagera Sugar ambao ni wenyeji zinatarajia kukutana siku ya Jumamosi ikiwa ni mwendelezo wa mechi zake za Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.

Akizungumza na DIMBA, Mexime alisema wanatambua kuwa wameanza vibaya ligi kuu msimu huu lakini haimaanishi kuwa watakuwa daraja mbele ya mabingwa hao watetezi wa ligi kuu msimu uliopita kwenye uwanja wao wa nyumbani.

“Naamini utakuwa mchezo mgumu lakini mashabiki wetu watambue kuwa ushindi wa kwanza kwa timu ya Kagera utaanzia kwa Yanga, nawafahamu vyema na najua fitina zao lakini hapa wasitegemee mteremko wowote, tumejiandaa vyema na tuna amini ushindi wa pointi tatu utaanzia nyumbani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here