Home Burudani (MFAHAMU SNOOP DOGG -47)

(MFAHAMU SNOOP DOGG -47)

1159
0
SHARE

Snoop Dogg: nilishindwa kuzima bifu la east coast, west coast

NA BADI MCHOMOLO

TUPO katika hatua za mwisho kumaliza historia ya rapa Snoop Dogg, leo hii ni sehemu ya 47 ikielezea maisha ya msanii huyo tangu akiwa na umri mdogo hadi hapo alipo na umri wa miaka 45.

Kutokana na mapendekezo ya wasomaji wengi wa safu hii, wamedai kuwa simulizi ijayo tumwelezee mkali wa ngumi za kulipwa duniani, Floyd Mayweather, ambaye mwezi uliopita alitangaza kustaafu ngumi, baada ya kumchapa mpinzani wake, Conor McGregor na kutwaa mkanda wa ‘Money Belt’.

Kwa kukukumbusha yale ya wiki iliyopita katika safu hii tuliona jinsi Snoop Dogg alivyoweka wazi kuwa hawezi kunywa chai bila kuwa na msokoto wa bangi pembeni, ili kuifanya chai hiyo kuwa tamu zaidi.

Snoop alisema ili chai yake iweze kuwa tamu zaidi, ni lazima kuwa na bangi pembeni, hata msokoto mmoja na kama atakosa kuwa na msokoto, basi ni bora asinywe kabisa chai hiyo.

Tuachane na mada hiyo, leo hii tunaangalia msanii huyo alivyoshindwa kumaliza tofauti za wasanii kutoka kundi la West Coast na East Coast.

Kwa kukukumbusha ni kwamba, ugomvi wa makundi hayo mawili ulianza katikati ya miaka ya 90, chanzo kikubwa kilikuwa rapa 2pac Shakur akiwa chini ya lebo ya Death Row Records iliyokuwa inamilikiwa na Dr Dre dhidi ya Notorious B.I.G akiwa kwenye lebo ya Bad Boy Records ikiwa chini ya rapa P. Diddy.

Death Row walikuwa wanatoka Los Angeles, ambao ni West Coast, kundi lao lilikuwa linaundwa na 2pac, Ice Cube, Eazy E, Dr Dre, Snoop Dogg, Mac Dre, Warren G, Nate Dogg, huku Bad Boys wakitoka New York, wakijulikana kwa jina la East Coast, wasanii wao walikuwa Nas, Notorious B.I.G. Jay-Z, LL Cool J, Big Daddy Kane, Kool G Rap, Big Pun, Big L na DMX.

Bifu lilianzia baada ya 2pac kugombana na rafiki yake, B.I.G, hivyo kusababisha makundi hayo na mashabiki wao kuanza kurushiana maneno kila kukicha.

Hali ilikuwa mbaya mitaani, hasa pale wanapokutana wapinzani hao, jambo ambalo lilikuwa linasababisha vifo kwa baadhi ya mashabiki kabla ya waasisi wa ugomvi huo, 2pac na B.I.G kupoteza maisha mwaka 1996 na 1997.

Hadi inafikia hatua hiyo ya waasisi kupoteza maisha, rapa Snoop Dogg alikuwa na wakati mgumu, huku akiamini kwamba, na yeye anaweza kupoteza maisha kutokana na mgogoro huo.

Katikati ya mwaka 1997, Snoop aliamua kumuita P.Diddy kutoka Bad Boys ili kuweza kumaliza tofauti zao za East Coast na West Coast.

“Niliona bora tukae pamoja ili kumaliza tofauti zetu, kikubwa niliona kwamba, watu wengi, hasa vijana wadogo walikuwa wanatuangalia sisi tunafanya nini katika muziki wetu, hasa katika mambo mazuri kwa jamii.

“Kwa upande wa P.Diddy, alisema kwamba hana tatizo lolote na sisi, lakini hana nafasi ya kumaliza tofauti hizo kwa kuwa kundi lina watu wengi, hivyo mbinu zangu za kumaliza tofauti hizo ziligonga mwamba,” alisema Snoop.

Tukutane Jumatano ijayo kwa ajili ya mwendelezo. Maoni, ushauri nitumie kwa namba 0714107464 au Email Badimchomolo@yahoo.com.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here