Home Habari MFARANSA AMWONGEZEA ‘MZUKA’ KAPOMBE

MFARANSA AMWONGEZEA ‘MZUKA’ KAPOMBE

4979
0
SHARE

NA JESSCA NANGAWE

BAADA ya Kocha Mkuu wa Simba, Pierre Lechantre kumpa majukumu beki wa timu hiyo, Shomari Kapombe, kumtumia kama kiungo, mwenyewe amesisitiza maamuzi hayo hayampi wakati mgumu, zaidi ya kumwongezea umakini na kuhakikisha anatekeleza vyema majukumu yake.

Akizungumza na DIMBA, Kapombe alisema amekuwa akitekeleza majukumu yake kama mchezaji, hivyo kubadilishiwa nafasi ya kucheza kwake haiwezi kumpa changamoto zaidi ya kujipanga jinsi ya kukabiliana na wapinzani wake.

“Ni kawaida kwenye mpira, mchezaji kila nafasi anatakiwa kucheza, kubadilishiwa nafasi kwangu naona ni sehemu ya mpira, kikubwa ni kuhakikisha naimudu nafasi ile na kutomwangusha mwalimu,” alisema Kapombe.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here