SHARE

Jessca Nangawe

WAKATI Ligi Kuu ikiendelea kupamba moto,Kocha wa Coastal Union, Juma Mgunda, amesema ugumu wa ligi hiyo unamfanya kushindwa kutabiri ubingwa huo utatua wapi msimu huu.

Simba ambao ni mabingwa watetezi wameendelea kutawala kileleni ba ada ya kujikusanyia pointi 50 mpaka sasa huku wakifukuziwa na wapinzani wao Azam pamoja na Yanga.

Akizungumza na DIMBA Jumatano,Mgunda alisema,msimu huu hali ya upinzani imeendeelea kutawala kwa timu  zote shiriki na kufanya kushindwa kutabiri ni timu gani inaweza kutwaa ubingwa huo.

“Kama ni mfuatiliaji mzuri,msimu huu kila timu inasumbua mwenzake, hakuna  wenye wachezaji wazuri ama la, kila mmoja anapambana kivyake kufanya vizuri, kwangu ukiniuliza nani atachukua ubingwa, naweza kusema hata Coastal yangu inaweza”alisema Mgunda.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here