Home Habari MIDO MBEYA CITY AIITA YANGA MEZANI

MIDO MBEYA CITY AIITA YANGA MEZANI

515
0
SHARE

NA MARTIN MAZUGWA,

KIUNGO wa kati wa timu ya Mbeya City, Raphael Daudi, amesema yupo tayari kukipiga kwa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Yanga, msimu ujao wa ligi.

Akizungumza na DIMBA, Daudi alisema kwamba yeye yupo tayari kucheza timu yoyote, lakini Yanga ndiyo timu anayoipa nafasi kubwa kutokana na kushiriki michuano ya kimataifa kwa miaka mingi sasa bila kukosa.

“Timu ambayo inahitaji huduma yangu ije tuzungumze, lakini bado naipa nafasi ya kwanza Yanga kutokana na kushiriki michuano ya kimataifa mara kwa mara.

Daud, ambaye hadi sasa amepachika jumla ya mabao tisa msimu huu, amekuwa ni msaada mkubwa kwa timu hiyo yenye maskani yake jijini Mbeya, ingawa amekuwa pia akiwindwa na baadhi ya timu, zikiwamo Simba na Yanga.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here