SHARE

LOS ANGELES, Marekani

LOLOTE linaweza kutokea katika ndoa ya Justin Bieber na bibiye Hailey Baldwin na hiyo ni baada ya bonge la fumanizi kupitia simu ya mkononi ya mshkaji.

Hailey amezinasa ‘laivu bila chenga’ meseji za jamaa alizokuwa akizituma kwa Selena, ambaye inafahamika kuwa ni mpenzi wake wa zamani.

Kwa mujibu wa mtandao wa RadarOnline, binti huyo, Hailey, alicharuka na hadi sasa hajarejea sawa kiakili, akiamini bado wawili hao ni wapenzi.

“Hailey amevurugwa kutokana na hilo,” kilisema chanzo kimoja na kuongeza kuwa binti huyo alichukua simu na kumpigia Selena, akimwambia ‘acheze anakochezaga’ na si kumkaribia mumewe huyo.

Cha kushangaza, inaelezwa kuwa Selena hakushtuka na badala yake alicheka tu, jambo linaloibua shaka kuwa huenda ni kweli bado hajaachana na Bieber.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here