Home Habari MKUDE AFICHUA SIRI YA KUSUGUA BENCHI

MKUDE AFICHUA SIRI YA KUSUGUA BENCHI

2341
0
SHARE

NA CLARA ALPHONCE

WAKATI baadhi ya wadau wa soka nchini wakiwa na maswali mengi kutokana na benchi la ufundi la Simba chini ya kocha wao, Mkuu Joseph Omog, kumsugulisha benchi nahodha wao wa zamani, Jonas Mkude, kiungo huyo ameibuka na kufichua siri nzito.

Si jambo la kawaida kwa Simba kumuweka benchi Mkude akiwa si majeruhi hasa kwenye michezo migumu kama wakikutana na Yanga, lakini hilo lilitokea hivi karibuni katika mchezo wa Ngao ya Jamii na hata ule wa ufunguzi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, dhidi ya Ruvu Shooting.

Akizungumzia hali hiyo, Mkude amesema hata wakati yeye akiwa katika kikosi cha kwanza, kuna wengine waliokuwa wakisubiri benchi, hivyo hali hiyo ndiyo inayomtokea lakini akaahidi atapambana kurejesha heshima yake.

“Ni kawaida tu, hata mimi nilipokuwa napewa nafasi, kuna wengine walikuwa wanakaa benchi kama hivyo, sioni kama kuna ajabu sana kwenye jambo hili.

“Kinachotakiwa kwa sasa ni kujituma kwa kufanya mazoezi ya nguvu na wenzangu na mengine ya ziada, ili kumshawishi kocha aweze kuniamini tena na kunipa namba,” alisema Mkude.

Alisema kikosi chao kwa sasa ni kipana, kina wachezaji wengi hivyo ni lazima mtu ujitume ili uweze kupata namba, tofauti na msimu uliopita.

Kukalishwa benchi kwa Mkude kumezua maswali mengi hasa kwa mashabiki wa Simba, wakimlaumu Omog kwamba anataka kuharibu kiwango cha kiungo huyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here