SHARE

NA MAREGES NYAMAKA,

WAKATI Azam FC wakitamba kuwa watawafanyia Simba kitu mbaya kama ilivyokuwa michuano ya Mapinduzi, nahodha wa wekundu hao wa Msimbazi, Jonas Mkude, amewaambia mashabiki wao kuwa wamiminike kwa wingi uwanjani kuona jinsi wanalambalamba hao watakavyoaibika.

Timu hizo mbili zitakutana mwishoni mwa wiki hii Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, mchezo unaosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa pande zote wakiwamo pia wa Yanga.

Ugumu wa mchezo huo unatokana na mambo mawili makubwa, moja likiwa ni kufukuzia mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara na jingine ni kutokana na matokeo ya michuano ya Mapinduzi ambapo Simba ilifungwa bao 1-0.

Mkude aliliambia DIMBA Jumatano kwamba, mchezo huo utakuwa mgumu lakini wamejipanga kuhakikisha wanapata matokeo mazuri ili kuzidi kujiimarisha kileleni.

2 COMMENTS

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here