Home Habari MLIMANI PARK WAFUNGUA MWAKA NA ‘NAISUBIRI BAHATI’

MLIMANI PARK WAFUNGUA MWAKA NA ‘NAISUBIRI BAHATI’

511
0
SHARE
NA JESSCA NANGAWE

BENDI kongwe ya muziki wa dansi nchini, Mlimani Park Orchestra ‘Sikinde Ngoma ya Ukae’, imefungua mwaka na ngoma mpya ‘Naisubiri bahati’ ambayo waliitambulisha kwa mara kwanza wakati wa sikukuu za mwishoni mwa mwaka.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Kiongozi wa bendi hiyo, Abdalah Temba, alisema wimbo huo umetungwa na mpiga dramu wao mkongwe, Habib Jeff, ambapo wakati wowote kuanzia sasa wataingia studio kuurekodi.

“Wimbo huu tayari tumeutambulisha kwa mashabiki wetu wakati wa sikukuu ya Krisimasi na mwaka mpya, tunashukuru umepokelewa kwa kishindo kwani wengi wameonyesha kuukubali na ndiyo maana tunakwenda kuurekodi ili kuwapa burudani zaidi,” alisema Hemba.

Aliongeza kuwa bendi hiyo imejipanga kuhakikisha mwaka huu unakuwa na mafanikio kwao katika kuleta mapinduzi ya muziki wa dansi ndani ya nje ya Tanzania kwa ujumla.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here